Sunday, March 23, 2008

Wajumbe wa serikali ya Uganda wanatarajiwa kusafiri Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini, Jumatatu ijayo katika awamu ya mwisho ya mazungumzo kati yake, na waasi wa Lord Resistance Army (LRA).

Mazungumzo hayo yatazingatia kumaliza ratiba ya utekelezaji; kuanda mkataba wa amani, na kuitia sahihi kutamatisha vita vilivyozidi miongo miwili.

Mapema mwaka huu, pande hizo mbili zilipiga hatua zilipomaliza agenda tano kuu, na kutia sahihi itifaki ya utekelezaji kufikia amani yenye kudumu.

Wiki jana serikali ya Uganda ilidai kiasi kikubwa cha wanamgambo wa LRA, waliondoka Garamba huko DRC wanakojificha, na kufika nchi ya Afrika ya Kati; kinyume na wanakotarajiwa kujikusanya na kujisalimisha huko Rikwangba, Sudan Kusini.

Ndio mkataba wa amani kutiwa sahihi, Joseph Kony anasema mashtaka dhidi yake huko ICC ni lazima yatupiliwe mbali, huku serikali ya Uganda inasema ni lazima atie sahihi mkataba huo kwanza, ili mashtaka dhidi yake kwa ICC yataweza kusahaulika.

Wiki mbili zilizopita, Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema hataikabidhi mahakama ya kimataifa ya jinai (ICC) viongozi wa LRA walioshtakiwa kwa makosa ya jinai, akidai wana-uganda wamekubali kutumia mahaka za Uganda pamoja, na mahakama ya kitamaduni inayoitwa Mato-oput.

0 comments: