Wednesday, March 19, 2008


Rais wa Libya, Muammar Al-Qathafi ameufungua msikiti mkubwa chini ya Sahara jijini Kampala, Uganda.

Msikiti huo unaoitwa Qathafi National Mosque, ulifadhiliwa naye (Qathafi) na unauwezo wa kuenzi watu kuzidi alfu ishirini kwa wakati mmoja.

Akifungua msikiti huo, Qathafi aliwasihi waislamu ulimwenguni kuwa kitu kimoja na kuzisahau tofauti za kidhehebu na kumheshimu maulana.

Waliohudhuria sherehe hiyo ni marais kutoka Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Mali, Djibouti, Zanzibar na waziri mkuu wa kwanza wa Tanzania.

Kabla hajaondoka Uganda, Qathafi anatarajiwa kupatana na marais hao.

0 comments: